Sunday, August 18

Wizara Ya Maji Yapokea Msaada Kutoka Benki Ya Dunia.

0


Serikali nchini kupitia wizara ya maji imepokea msaada wa dola za kimarekani milion 300 kutoka benki  ya dunia kwa lengo la kuwanufaisha wananchi kupata huduma bora ya maji sfi hususani maeneo ya vijijini.

Hayo yamezungumzwa na waziri wa maji Mhandisi Isaac Kamwelwe Jumanne hii  wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji yalioanza march 16 mwaka huu yenye lengo la kutathimini hali ya upatikanaji wa maji hapa nchini.

Mbali na hayo waiziri huyo ametoa neon la shukranio kwa  benki kuu ya dunia kwa msaada huo pamoja mna kueleza miradi mbali mbali ambayo itajengwa katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam, ikiwa ni pamoja na mradi wa kutibu maji taka wa utakaojengwa Mbezi Beach.

“Lakini pia Wakorea wametupatia fedha, tunajenga mtambo wa kutibu maji taka wa jangwani. Benki ya maendeleo ya Afrika nao wametupatia fedha, tunajenga mtambo wa kutibu maji Kurasini” Ameongeza Mhandisi Kamwene.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.