Sunday, August 25

Wawili wafariki Dunia kwa ajali ya gari Arusha

0


Na mwandishi wetu Arusha

Simanzi vilio na majonzi vimetawala baada ya watu   wawili kufariki dunia na watano kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Oldonyosambu wilayani Arumeru kwenye barabara kuu inayotoka mjini Arusha kuelekea Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya .

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Jonathan Shanna amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa 9 alasiri baada ya magari aina Toyota Saloon na Mitsubishi Saloon kugongana wakati gari moja likiwa linataka kuelekea eneo la Ngarenanyuki na lingine likijaribu kulipita.

“Ni kweli tukio limetokea majira ya saa 9 leo,Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani yupo eneo la tukio tunawapa taarifa kamili baadaye”aliongezea.

Hata hivyo kamanda huyo alisema majeruhi wa ajali hio wapo katika Kituo cha Afya Oldonyosambu wakiendelea na matibabu na miili ya marehemu ipo katika hospitali ya Mount Meru,”amesema Shanna

Waliofariki dunia katika ajali hiyo ni Reuben Mkunya raia wa Kenya na Peter Mushi mkazi wa Moshono jijini Arusha.

Share.

About Author

Leave A Reply