Sunday, August 25

Wakiristi ulimwenguni wakesha wakimkumbuka Yessu

0


Na mwandishi wetu

Mamia ya waumini wa dini ya  kristu wameshiriki ibada ya mkesha wa kusherehekea kufufuka kwa Yesu katika kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam usiku wa kumkia leo.

Ibada hiyo iliongozwa na Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Eusebius Nzigirwa ambapo wakristo wote duniani wanakumbuka kufufuka kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Wakati wa mahubiri   yake, Askofu Nzigirwa aliwataka waumini kutokuwa na hofu na kujua thamani ya nguvu ya ufufuko wa Yesu Kristo.

Alisema Pasaka sio siku ya watu wenye hofu tena kama Yesu aliweza kushinda mauti basi na sisi tunaoamini tutegemee kushinda kama ambavyo alishinda mokozi wetu Yesu Kristo.

Kufufuka  kwa Yesu ni kwaajili yetu na kunatuonyesha ni namna gani alidhibitisha kile alichokisema kabla ya kufa kwake hivyo tunapaswa kuwa na imani.

Katika ibada hiyo iliambatana na waumini kuwasha mishumaa ikiwa ni ishara ya kufufuka kwa Yesu Kristo.

 

Imehaririwa na Mohamed Khamis

Share.

About Author

Leave A Reply