Sunday, August 25

Rais Wa Nigeria Kutohudhuria Mkutano Wa AU.

0


Katika kikao cha wakuu wa nchi za umoja wa Afrika AU kinachofanyika wiki hii jijini Kigali nchini Rwanda, Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari hatahudhuria kikao hicho hatua ambayo imekuwa pigo katika mpango wa kuzindua na kutia saini mkataba wa biashara huruia kwenye nchi wanachama 54 ya umoja huo.

Mkutano wa juma hili jijini Kigali ulilenga kuzindua rasmi mkataba wa biashara huria kwa bara la Afrika, mkataba ambao baraza la mawaziri la Nigeria liliuridhia Jumatano ya wiki iliyopita.

Rais Buhari alitarajiwa kuondoka mjini Abuja Jumatatu ya wiki hii kuhudhuria sherehe za siku ya Jumatano, lakini akajiondoa kwa kile alichodai nchi yake inahitaji majadiliano zaidi kabla ya kuutia saini.

Taarifa ya ikulu ya Nigeria imesema kuwa “Rais hatasafiri tena kwenda Kigali kwaajili ya shughuli hiyo kwa kuwa baadhi ya wadau nchini mwake wamedai kuwa hawakushirikishwa na kwamba wanayomasuala yanayowagusa kwenye mkataba huo,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa “Uamuzi wa rais Buhari ni kwa lengo la kutoa muda zaidi wa kufanyika kwa majadiliano ya kina kuhusu mktaba huo.”

Miongoni mwa wadai waliomtaka rais Buhari kutotia saini mkataba huo ni pamoja na shirikisho la wafanyakazi.

Taasisi mbalimbali za wafanyakazi nchini humo zimedai kuwa mkataba huo utaenda kupigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la uchumi wa nchi hiyo ambao tayari unayumba.

Umoja wa Afrika uliamua kuendelea mbele na mkataba huu mwaka 2012 uliolenga kuanzishwa kwa soko la pamoja kwaajili ya ubadilushanaji wa bidhaa na huduma.

Mkataba huu unatengeneza majadiliano ya kimfumo ili kupanua biashara za ndani kuanzia kwenye ngazi ya chini kabisa kwa asilimia 14, imesema taarifa ya rais Buhari.

Nchi ya Nigeria ambayo ni mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika ina jumla ya idadi ya watu milioni 190 na ina soko kubwa.

Jumla ya wakuu wa nchi 26 wanatarajiwa kuhudhiria shughuli za utiaji saini mkataba huu jijini Kigali.

Umoja wa Afrika unasema soko la pamoja lipo kwenye agenda ya mwaka 2063, kuhusu muungano wa baraa la Afrika, ambapo Afrika itakua na sauti moja katika kuimarisha biashara kati ya bara hilo na mabara mengine.

Takwimu zinaonesha kuwa biashara kati ya nchi za afrika ni asilimia 16%.

Mkataba huu ambao utahusisha nchi wanachama 54 zenye idadi ya watu zaidi ya bilioni 1 utasaidia kuongeza biashara ya ndani ya bara hilo kwa zaidi ya asilimia 14 iliyopo kwa sasa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.