Sunday, August 25

Raia wa kigeni anaswa na shehena ya unga uwanja wa ndege Dar

0


Na mwandishi wetu Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege wa Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kimefanikiwa kumtia mbaroni  raia wa Latvia,Linda Mazure(22) akituhumiwa kuwa  na dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 5.091 alizokuwa akisafirisha kwenda nchini Poland.

Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege Tanzania,Jeremiah Shila alisema raia huyo alikamatwa Aprili 17 mwaka huu saa 9 mchana katika uwanja huo wa ndege na akiwa  ameficha dawa za kulevya h mabegi mawili ya nguo .

Alisema  mtuhumiwa huyo alikamatwa kwenye uwanja wa JNIA akiwa anajiandaa na safari ya kwenda nchini Poland kwa usafiri wa Shirika la Ndege Qatar  kupitia mji wa Doha.

Alielesa kuwa  mtuhumiwa huyo alikuwa na hati ya kusafiria yenye namba LV5893769 iliyotolewa Aprili 6 mwaka 2018.

“Polisi wetu kwa kushirikiana na maofisa wa usalama uwanja wa JNIA walimkamata Linda akiwa eneo la abiria la ukaguzi wa awali Teminal II na alipopekuliwa  alikutwa ameficha dawa hizo kwenye mabegi yake mawili ya nguo.

Hata hivyo alieleza kuwa   raia huyo anaendelea kushikiliwa na polisi wa kituo cha JNAI kwa ajili uchunguzi zaidi na uchunguzi utakapokamilika  atafikishwa Mahakamani.

Hata hivyo alitoa  onyo kwa watu wanaojihusisha nan a biashara ya dawa za kulevya,nyara za serikali,utoroshaji wa madini na uharifu wa aina yeyote kwa kutumia viwanja vya ndege waache kwani wakibainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

 

Imehaririwa na Mohamed Khamis

Share.

About Author

Leave A Reply