Friday, August 23

Mzee Mwenye Miaka 90, Akamatwa Kwa Ubakaji.

0


Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 90 aliyefahamika kwa jina la Kachuka Malongo mkazi wa mkoani Shinyanga, ameshikiliwa na Jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za kuwabaka wanafunzi watano wa shule ya msingi kwa nyakati tofauti tofauti.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule wakati akizungumza na wanahabari, amesema wanafunzi hao wenye umri wa miaka minane hadi 12, alikuwa akiwarubuni kwa kuwapa pipi na pesa, kutokana na uchu wa mapenzi aliokuwa nao.

“Tumebaini chanzo cha tukio hilo kuwa ni tamaa na uchu wa mapenzi, kwa hiyo tunamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi na uchunguzi ukikamilika tutampeleka mahakamani”, amesema Kamanda Haule.

Aidha amesema taarifa za watoto hao kufanyiwa vitendo hivyo vya ukatili zilitolewa na mkazi wa eneo hilo analoishi mzee huyo, na kwamba polisi waliamua kuzifuatilia na kumkamata mtuhumiwa huyo.
Kamanda Haule amewataka wazazi kuwa makini na karibu na watoto wao, ili kubaini matatizo yao au jambo lolote linapowatokea.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.