Thursday, August 22

Mwanzilishi Wa Facebook Aomba Radhi Kwa Kuingiliwa Taarifa Za Watumiaji.

0


Mark Zuckerberg mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook ameibuka na kudai kwamba wamefanya makosa, ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa kashfa ya Cambridge Analytica. Analytica inatuhumiwa kuingilia data za watumiaji million 50 wa mtandao wa Facebook.

Katika ujumbe wake kupitia ukurasa wake wa Facebook Zuckerberg amesema kitendo hicho kimewavunjia uaminifu kwa watumiaji wa mtandao ho na, hivyo kutokana na hali hiyo ameahidi kufanyika mabadiliko kadhaa ili kutoingiliwa tena na kuibwa kwa taarifa za watumiaji wake.

“Tuna wajibu wa kuzilinda taarifa zenu,na kama tukishindwa kuzilinda hatuna sifa ya kuwahudumia,mimi ndiye niliyeanzisha mtandao huu wa Facebook,mwisho wa siku nina wajibika kwa chochote kinachotokea katika mtandao wetu.” Amesema Zuckerberg.

Aidha, Katika kufuatilia matatizo ya sasa na ya zamani amesema atafanya mambo yafuatayo

  • Kuchunguza mitandao yote ambayo inashirikiana na uga wa Facebook kabla ya kufanyiwa mabadiliko yam waka 2014 ya namna ya kuweza kupata taarifa ya watumiaji.
  • Kufanyia uchunguzi kazi za program za kimitandao zinazotiliwa shaka.
  • Kupiga marufuku mwanzilishi wa program yoyote ambayo inagoma ama haitoi ushirikiano katika uchunguzi pamoja na hatua nyingine ambazo wanaona zita pafanya Facebook kuwa mahala salama.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kimitandao wanasema kwamba Facebook hawapo tayari kuomba radhi kwa kile kilichotokea, na tena hakuna maelezo yoyote kwa wizi wa taarifa zake uliofanyika mwaka 2014, ambapo ulikuwa ni wakati muafaka kuchukua hatua sitahiki.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.