Wednesday, August 21

Mkosoaji Wa Rais Akamatwa-Zambia.

0


Mkosoaji huyo wa rais Edgar Lungu anayefahamika kwa jina la Chishimba Kambwili ambaye aliwahi kuwa Waziri wa zamani wa Zambia, amekamatwa jijini Lusaka kwa tuhuma za kujipatia faida kupitia mtandao wa kihalifu.

Aidha, Kambwili ambaye amekamatwa Alhamisi ya wiki hii, hivi karibuni ameibuka kuwa kinara na mkosoaji mkubwa wa Lungu ambaye anakosolewa kwa kuongoza nchi hiyo kiimla na kuwakamata wapinzani wake.

Keith Mweemba ambaye ni Wakili wa Kambwili, amesema ameshtakiwa kwa jumla ya makosa 37, liliwemo la kuwa na mali ambazo upatikanaji wake umetokana na uhalifu, na kwamba Kambwili alizuiliwa na polisi na alitarajiwa kupelekwa mahakamani Ijumaa hii.

Kambwili ni mbunge kutoka chama tawala cha Patriotic Front, aliwahi kuwa waziri mambo ya nje, pia aliwahi kuhudumu kama waziri wa habari chini ya utawala wa rais Edgar Lungu.

Tangu kutolewa katika nafasi yake ya uwaziri, ametofautiana na rais Lungu na mara zote amekuwa akimtuhumu rais na Serikali yake kuwa ni ya kifisadi.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.