Saturday, July 20

Mamlaka za Maji Zatakiwa Kutumia TEHAMA Kuimarisha Ukusanyaji wa Mapato

0


1

Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akisisitiza umuhimu wa Watendaji  Wakuu wa Mamlaka za Maji na Wahandisi wa Maji Mikoa kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao kwa weledi ili kutimiza  azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha kuwa wanawafikisha huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.hayo yamejiri  leo Jijini Dodoma wakati wa akifungua Kikao kazi cha siku mbili kwa watendaji hao leo Jijini Dodoma.

2

Naibu Waziri wa Maji mhe. Jumaa   Aweso akizungumzia umuhimu wa watendaji wakuu wa Mamlaka za maji  na wahandisi wa mikoa kusimamia miradi ya maji inayotekelezwa katika maeneo yao  kwa kuzingatia uzalendo na uadilifu.

3

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akizungumza  wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Watendaji wakuu wa Mamlaka za Maji na Wahandisi wa maji wa Mikoa, kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku mbili.

4

Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Mamlaka za Maji na Wahandisi wa maji wa Mikoa  yote hapa nchini.

5

Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja  (katikati) akiwa na watendaji wengine wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Watendaji wakuu wa Mamlaka za Maji na wahandisi wa mikoa leo Jijini DODOMA.

6

Sehemu ya washiriki  wa kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Mamlaka za Maji na Wahandisi wa maji wa Mikoa  yote hapa nchini wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufungua kikao kazi hicho cha siku mbili.

7

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Emmanuel Kalobelo akizungumza wakati wa hafla ya kufungua  kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Mamlaka za Maji na Wahandisi wa maji wa mikoa .

8

Sehemu ya washiriki wa Kikao kazi cha Watendaji wakuu wa Mamlaka za maji na Wahandisi wa maji wa mikoa kinachofanyika kuanzia leo Jijini Dodoma.

9

Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na sehemu ya washiriki wa Kikao kazi cha siku mbili kinachowashirikisha watendaji wakuu wa Mamlaka za maji na Wahandisi wa mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma.

(Picha na Frank Mvungi- MAELEZO

………………

Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma

Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa amewataka Watendaji wakuu wa Mamlaka za Maji na Wahandisi wa Maji kuhakikisha wanatumia  mifumo ya TEHAMA katika kukusanya mapato ili kuongeza ufanisi katika mamlaka hizo.

Akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili kinachowashirikisha Watendaji wakuu wa Mamlaka za maji na Wahandisi wa maji wa mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma chenye lengo la kujenga uwezo kwa watendaji hao ili  kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na huduma ya majisafi na salama.

“Matumizi ya TEHAMA yatasaidia Mamlaka zote kuongeza mapato yake hali itakayosaidia kuimarisha huduma zinazotolewa kwa wananchi kwa kutumia fedha zitakazokusanywa na dhamira yetu kama Viongozi ni kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika na huduma hii”; Alisisitiza Mhe. Prof. Mbarawa

Akifafanua amesema kuwa Baadhi ya Mamlaka zimeanza kutumia mifumo hiyo na imeonyesha mafanikio makubwa kwa kuongeza mapato kutoka wastani wa Bilioni 8.2 hadi bilioni 10.1 kwa sasa yakiwa ni mafanikio ya kupigiwa mfano.

Akizungumzia utekelezaji wa miradi  ya maji isiyoridhisha Prof. Mbarawa amesema Serikali haitatoa kazi kwa mkandarasi  ambaye ameshindwa kutekeleza mradi aliopewa ili iwe fundisho kwa wakandarasi wengine.

Kuanzia sasa mkandarasi atakayeshindwa kutekeleza mradi wa maji katika eneo lolote hapa nchini asitarajie kupata kazi za miradi ya maji katika eneo lolote hapa nchini ili kuleta nidhamu kwa wale wanaopewa miradi.

Pia, Waziri Mbarawa ameagiza Mamlaka za Maji kutenga sehemu ya mapato yake kwa ajili ya kupanua huduma zake kwa wananchi.

Aidha, Waziri Mbarawa amebaisnisha kuwa Serikali imewekeza kiwango kikubwa cha fedha kwa ajili ya miradi ya maji ikiwemo katika Jiji la Dar es Salaam ambapo bilioni 800 zimewekezwa, Arusha bilioni 500 na mradi wa Shinyanga Tabora Nzega takribani bilioni 600.5 zinatumika katika utekelezaji wa mradi huo.

“Kwa upande wa watendaji wa Mamlaka za Maji na Wizara hiyo Prof. Mbarawa amesema kuwa mhandisi si kupata degree bali kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi yatakayosaidia wananchi kupata maji safi na Salama”; Alisisitiza Mhe. Prof. Mbarawa.

Wizara ya Maji imekuwa ikichukua hatua za makusudi katika kuhakikisha kuwa kila mtanzania anafikiwa na huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wote, Kikao Kazi cha Watendaji wakuu wa Mamlaka za Maji na Wahandisi wa mikoa ili kujenga uwezo wa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Share.

About Author

Leave A Reply