Sunday, August 18

“Lipumba si Mkweli”-Maalim Seif.

0


Maalif  Seif Sharif  Hamad katibu Mkuu wa Chama Cha wanachi CUF,  amesema Mwenyekiti wa Chama hicho Prof. Ibrahimu Lipumba anayeungwa mkono na Msajili wa Vyama vya siasa, anatakiwa kuacha kukivuruga chama hicho kwani muda walionao kwa sasa ni kukijenga chama.

Maalim ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wake na wanachama wa chama hicho uliofanyika katika Hoteli ya Korini iliyopo Tandale jijini Dar es Salaam ambapo amewataka wanachama wake kuwa wamoja na kutoyumbishwa na upande wa Lipumba.

Amesema kuwa Lipumba ni mtu asiyekuwa mkweli, kwani yeye ndiye aliyempokea Edward Lowassa katika UKAWA lakini siku chache baadae akageuka na kudai kuwa hakubaliani na maamuzi ya kumkaribisha katika umoja huo.

Mkutano baina ya Katibu mkuu wa chama hicho na wanachama hao ulikuwa na lengo la kujenga mshikamano na umoja ndani ya chama hicho.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.