Wednesday, August 21

Hali Mbaya Kwa Urusi: Ujerumani, Marekani, Australia Kuwafukuza Wanadiplomasia Wa Urusi.

0


Serikali ya Ujerumani imetangaza kuwafukuza wanadiplomasia wanne wa Urusi kuhusiana na shambulio la sumu dhidi ya jasusi wa zamani wa Urusi, Sergei Akripal na mwanawe wa kike Yulia, nchini Uingereza.

Urusi bado haijatoa maelezo kuhusiana na shambulio hilo, imesema wizara ya mambo ya kigeni kuptia ukurasa wa Twitter na kuongeza kwamba wizara hiyo inataka kuonesha ishara ya mshikamano na Uingereza.

Hatua hiyo ya serikali imesifiwa hata na upinzani, ambapo mbunge wa chama cha walinzi wa mazingira Green, Robert Habeck amesema kwa kuwa Urusi imezuwia juhudi za kujieleza kile kilichotokea mjini Salisbury, ni jukumu la Putin kuipoza hali hiyo na kushiriki katika uchunguzi wa uhalifu huo. Mataifa mengine 15 ya Umoja wa Ulaya, pamoja na mataifa mengine ya magharibi, yamesema yatachukua hatua kama hizo, baada ya Uingereza kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Urusi mapema mwezi huu.

Waziri mkuu wa Australia ametangaza leo kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi. Marekani imechukua hatua ya kuwafukuza wanadiplomasia 60, lakini balozi wa Urusi nchini Marekani, Anatoly Antonov, ameiita hatua hiyo kuwa ni potofu na kuonya itachafua kwa kiasi kikubwa uhusiano kati ya Urusi na Marekani.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.