Monday, August 19

Faru Sudan Wa Kiume Na Wa Mwisho Duniani Afariki.

0


Watafiti wanasema Faru mweupe wa mwisho wa kiume duniani anayejulikana kwa jina la Sudan amefariki kufuatia matatizo aliyokuwa nayo yaliyochangiwa na umri wake. Taarifa kutoka hifadhi ya wanyama ya Ol Pejeta nchini Kenya imesema faru huyo aliyekuwa na umri wa miaka 45 alidungwa sindano afe jana Jumatatu baada ya hali yake kiafya kuwa mbaya zaidi hadi kufikia hatua ya kushindwa hata kusimama. Faru huyo alikuwa ni moja ya matumaini na juhudi za kuendelea kulinda Faru hao wasitoweke kwa msaada wa Faru wengine wawili wa kike. Faru Sudan alikuwa ni balozi mzuri na atakumbukwa kwa kazi aliyofanya ya kuhamasisha juu ya madhila siyo tu yanayowakabili Faru pekee bali pia jamii ya wanyama wengine walio katika hatari ya kutoweka kutokana na shughuli zinazofanywa na binaadamuRead More

Share.

About Author

Comments are closed.