Friday, July 19

Bungeni: Serikali inafuatilia stahiki za Mtanzania aliyetunga wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

0


Serikali imesema bado inafuatilia malipo ya John Joseph aliyetunga wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Damas Ndumbalo amesema tayari Serikali imeshawasilisha ombi la madai kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na wanasubiri majibu.

“Tulipokea barua kutoka wizara ya habari kuhusu Mtanzania aliyetunga wimbo huo akidai stahiki zake, tayari tumepeleka kwenye jumuiya na wenzetu wanapitia kuona kama kulikuwa na makubaliano yoyote ili waweze kuyafuata,” amesema Dk Ndumbaro

Amlitoa kauli hiyo bungeni leo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Martha Mlata aliyetaka kujua stahiki za Mtanzania huyo kutoka mkoani Kagera.

Katika swali la msingi, Mlata alihoji Tanzania ilishiriki namna gani katika mchakato wa kuupata wimbo maalum wa Afrika Mashariki.

Naibu waziri huyo alisema Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi tatu waanzilishi wa EAC ikiwamo Uganda na Kenya na ndizo zilianzisha mchakato wa kuupata wimbo wa jumuiya.

Alizitaja hatua mbalimbali zilizopitiwa katika kuupata wimbo huo hadi kuupata mmoja uliokubaliwa na kuruhusiwa

Share.

About Author

Leave A Reply