Sunday, August 25

AL-Qaeda Wadai Kuhusika Na Shambulio Lililoua Watu 14.

0


Kundi la Al-Qaeda lenye uhisiano na wapiganaji wa Al-Shabab nchini Somalia limekiri kuhusika kwenye shambulio lililotokea jana Alhamisi wakati gari lilipolipuka nje ya hoteli moja maarufu ijini Mogadishu ya Weheliya iliyopo katikati mwa mji huo. Mogadishu,

Msemaji wa Serikali Abdiazis Ali Ibrahim, amesema watu 14 walipoteza maisha kwenye eneo la tukio na kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka wakati huu vikosi vya uokoaji vikiendelea kutafuta miili zaidi ambapo taarifa kutoka kundi hilo zinadai kuwa lililenga mkutano wa viongozi wa Serikali.

Watu walioshuhudiwa tukio hilo wanasema ulitokea kwenye mtaa wa Makkah al-Mukarama moja ya mitaa ambayo inashughuli nyingi kuunganisha na eneo la kati la mji wa Mogadishu.

Mji wa Mogadishu umekuwa ukilengwa na mashambulizi ya mara kwa mara yanayotekelezwa na kundi la Al-Shabab linalopigana kuiangusha Serkali ya Somalia inayotambuliwa kimataifa.

Mwaka 2015 Hoteli hiyo hiyo ya Weheliya ilishambuliwa na wanagmabo wa Al-Shabab. Shambulio jingine baya kwenye mji huo lilikuwa ni mwezi Februari ambapo watu zaidi 38 walipoteza maisha mjini Mogadishu.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.