Tuesday, July 23

Tumia Android Au iOS Kama Mouse Katika Kompyuta!

0


‘Mouse’ ni kitu cha msingi sana katika Kompyuta, lakini kazi nyingi za kompyuta hata simu janja zinafanya siku hizi. Kama kawaida yetu TeknoKona huwa tunakuletea habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia, na leo tunakuja na Remote Mouse.

Hivi ni mara ngapi umekuwa unataka kutumia kompyuta yako bila bugudha na ukashinda? fikiria ukitaka tumia kompyuta ukiwa kitandani! 😆  … simu yako inaweza ikawa ndio suluhisho la hilo jambo

App: Remote Mouse

App ambayo tunakuwekea mezani leo ni App inayojulikana kama Remote Mouse, ili kuifanya ifanye kazi fuatilia maelekezo haya

  • Ishushe Hapa  PlayStore   AppStore kupitia simu janja yako au tabiti.
  • Ukishamaliza, Sasa nenda kashushe Remote Mouse katika Kompyuta yako. Kufanya hivyo ingia katika mtandao huu na kisha shusha kulingana na aina ya kompyuta ambayo unayotumia.
  • Baada ya hapo inakubidi uunganishe kifaa chako (simu/tabiti) na komypyuta kwa kutumia WiFi
  • Fungua Remote Mouse katika simu yako na kisha chagua jina la Kompyuta yako katika listi ya majina ili kuunganishwa.
Mfano: Jina La Kompyuta Likitokea Katika Listi Chaguzi Za Kompyuta

Mfano: Jina La Kompyuta Likitokea Katika Listi Chaguzi Za Kompyuta

  • Baada ya hapo utapata utambulisho mfupi na kisha ‘Mouse’ itaonekana, na itakuwa tayari kwa kutumia.

Ukiachana na hilo pia App unaweza ukaitumia kama ‘keyboard’ ya kompyuta  kabisa kwa kuchagua kialama cha ‘keyboard’ pia njia za mkato kama Windows, ctrl, alt n.k unaweza ukazipata kwa urahisi kabisa ndani ya App.

Muonekano Wa App Ya 'Remote Mouse'

Muonekano Wa App Ya ‘Remote Mouse’

Kingine kizuri kabisa ni kwamba unaweza ukafanya vitu vingi sana kama  kuzima kompyuta, kuongeza sauti na kupunguza sauti, kuilaza, kui’restart’  na kuizima kompyuta n.k ndani ya App.

Mpaka sasa nadhani unaweza ukatumia Remote Mouse. Tembelea TeknoKona kila siku kwa maujanja kama haya na habari kedekede za kiteknolojia. Kumbuka, TeknoKona daima tupo nawe katika teknolojia.

Share.

About Author

Leave A Reply