Monday, June 24

Kujua IMEI ya simu iliyopotea au kuibiwa. #Maujanja #Android #iPhone

0


IMEI namba ni kitu muhimu sana wakati pale simu janja yako imeibiwa au umepoteza na unataka kufanya jitihada za kuipata tena. Kwa polisi ni lazima utapeleka na taarifa IMEI ya simu husika. Vilevile, kama una mpango wa kui’track simu hiyo ndio njia mojawapo.

Ni wazi kwamba inajulikana ukiwa na kifaa chako unaweza ukapata IMEI ya simu yako baada ya kupiga *#06#  katika simu yako. Ssasa kama hilo linawezekana hivyo vipi ukiibiwa kifaa chako hicho?

IMEI kwa kirefu chake ni ‘International Mobile Equipment Identityambayo wa haraka ni namba ambazo zinakuwa kama utambulisho wa kifaa na katika simu mara nyingi zinakuwa 15. Namba hizi huwa hazifanani na zinakuwa katika kifaa kimoja tu.

Faida yake inakuja pale unapokuwa umepoteza kifaa chako, kwa sababu namba hiyo ni moja tu kwa kifaa kile hivyo itakuwezesha kuweza kufuatilia nyendo za simu hiyo kama ikiwa imeunganishwa na intaneti.

Ukiachana na kuipata simu janja hiyo. Vilevile, unaweza ukaamua kufuta kila kitu na kuifunga kabisa simu hiyo kutoweza tumika tena kupitia IMEI ya simu hiyo.

JINSI YA KUPATA IMEI YAKO KAMA HUNA KIFAA CHAKO

Kama huna simu janja yako karibu na wewe unaweza ukapta IMEI kwa kutumia Find my device kwa wale wa Android na Find My Phone kwa wale wanaotumia vifaa vya Apple.

Android.

kujua IMEI

Kujua IMEI kwenye simu ya Android

Kwa watumiaji wa Android ni kwamba unaweza kupata IMEI yako kwa kutumia akaunti ya Google ambayo ulikua umeiweka katika simu yako (uliyokua unatumia katika PlayStore).

  • Kwa kuingia katika Android Device Manager kwa kutumia kompyuta
  • Ingia kupitia akaunti yako ya Google ambayo ulikua unaitumia katika simu yako.
  • Ukifanikiwa kuingia humu utaona vifaa vyote ambavyo vimeungwa na akaunti hiyo, unaweza chagua kifaa husika na kuone taarifa zake ikiwemo IMEI.

Apple.

kujua imei

Kujua IMEI kwenye iPhone

Kwa kutumia kompyuta yako ingia katika tovuti ya Apple 

  • Ingia katika Akaunti yako kwa kutumia Apple ID
  • Ukishaingia nenda katika orodha ya vifaa kisha chagua jina la kifaa
  • Taarifa za kifaa husika zitatokea ikiwemo na IMEI ya kifaa hicho.

Hizi ndio njia ambazo zinafanya kazi katika simu zote za Android na iPhone. Hivyo nadhani zile kesi za kuacha kufuatilia kifaa chako kisa umesahau IMEI hazitakuwepo tena.

Kuna wengine hata kwenda Polisi kutoa ripoti ya kuibiwa simu zao kisa wanasema wataulizwa IMEI za vifaa vyao na wao hawana hifadhi/kumbukumbu ya IMEI.

Tembelea TeknoKona Kila Siku Kujipatia Maujanja Kedekede Ya Teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Share.

About Author

Leave A Reply