Wednesday, August 21

Huawei Yasema Imejipanga Vyema Licha Ya Kuwakosa Google!

0


Licha ya kampuni ya Huawei kushutumiwa na vita ya kiusalama ambayo imepelekea kampuni hiyo kukosa ushirika na baadhi ya makampuni mengine kama vile Google na Qualcomm, bado imeinua kifua mbele na kusema jambo hilo bado halitawarudisha nyuma kama watu wengi wanvyodhani.

Bwana, Ren Zhengfei amabe ndio mwanzilishi wa Huawei amesema kuwa kampuni yake licha ya kupata changamoto kama hizo bado itajikita zaidi katika kujiendeleza na kuzidi kuwa juu kwa sababu wana mikakati mingi sana ili kufanikisha hilo.

Logo Ya Huawei Na Logo Ya Google

Logo Ya Huawei Na Logo Ya Google

“Katika kipindi hichi kigumu napenda kushukuru makampuni kama vile Google na mengine kadha wa kadha ambayo kwa namna moja yameisaidia Huawei kukua na kujiendeleza” – Ren, aliongezea.

Mkuu wa Huawei pia alishawahi sema kuiunga mkono na kuisapoti kampuni sio lazima mtu anunue simu toka katiaka kampuni hiyo. Hata yeye ana jamaa ambao wanatumia simu zingine lakini wanamuunga mkono yeye na kampuni yake.

Mkuu wa Huawei huwa sio mtu ambae anapendelea kuonekana na jicho la jamii akiwa anafanya mahijiano (interview) lakini safari hii anakiri kulikua hakuna jinsi kwani mambo mengi yalikuwa yantokea katika kipindi cha muda mfupi.

Moja Kati Ya Ofisi Za Huawei

Moja Kati Ya Ofisi Za Huawei

Kumbuka Huawei bado iko katika namba mbili kama mtengenezaji na muuzaji wa simu janja, baada ya kushika namba mbili ndio kashfa hii ikaja, baada ya hiyo Google nao wakaamua hivi lakini bado kampuni imeweka kifua mbele kuonyesha kwamba hivi ni vitu vya kawaida sana katika biashara.

Ifahamike kwamba Huawei hawategemei tuu katika biashara ya kutengeneza na kuuza simu tuu,  bado wana biashara zingine kama vile kuuza teknolojia n.k.

Je kwa hali ilipofikia sasa, wewe unaona bado Huawei bado wana uwezo wa kuhimili hali ya soko na kuendelea kubaki namba mbili nyuma ya Apple na mbele ya Samsung?

Tembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Ndio Mtandao Namba Moja Kwa Habari Na Maujanja Yote Yanayohusu Sayansi Na Teknolojia!.

Share.

About Author

Leave A Reply