Thursday, August 22

CIA Kujiunga Na Mtandao Wa Instagram!

0


vodacom swahili

CIA ukiachana na kazi yake ya kuhakikisha ulinzi na usalama upo tena kwa hali ya juu kabisa bado imeona sio vibaya kujisogeza na watu karibu zaidi kwa kutumia mtandao wa kijamii.

CIA wamesema kuwa wamewaomba washirika wenzao wa Instagram katika kuwasaidi kuanzisha akaunti hiyo, na Insta wamekubaliana na jambo hilo.

Kwa sasa wana Twitter hata na Facebook lakini wametoa tamko kuwa kiu yao itakatika pale watakapofunguliwa na akaunti ya instagram.

CIA

Ukiachana na kuwa chombo ambacho kwa namna nyingine kinaogopwa na kuheshimika sana, unaweza ukasema hata vitu ambavyo watapost vitakua ni vya watu fulani tuu (tabaka) lakini hapana. Chombo bado kinaweza kika post utani kama hivi ….

Haifahamiki tuu kwamba ni muda gani akaunti hiyo itakua tayari, lakini ni wazi kwamba akaunti hiyo itatumika katika kufundisha, kuburudisha na kukemea maovu.

Kumbuka siku hizi mitandao ya kijamii katika chaguzi mbalimbali imekua mstari wa mbele kuhakikisha kuwa uchaguzi unamalizika salama na kwa haki.

FBI na TSA wana akaunti katika mitandao ya kijamii, lakini kwa kiasi kikubwa FBI wanaboa 😥  hivyo ndio watu wanavyosema, lakini kwa kujipanga huku sidhani kama CIA watakua hivyo.

Endelea kuwa nasi, tutakujulisha CIA wanatumia jina gani katika mtandao huo.

Tembelea TeknoKona na mitandao yetu ya kijamii kila siku ili kujipatia habari za kiteknolojia. kumbuka daima tupo nawe katika teknolojia.!

Share.

About Author

Leave A Reply