Sunday, August 18

CIA: Huawei Wanapokea Msaada Wa Kifedha Kutoka Mashirika Ya Ulinzi Na Usalama!

0


vodacom swahili

Ukiachana na kuwa kampuni kubwa ya mawasiliano huko nchini china, kampuni hii bado inashikilia namba mbili — ambao  ipo katikati ya Apple na Samsung–  hili lilitokea baada ya Huwei kuipita Apple kiamuzo ya simu na kuchukua nafasi yake ya pili.

Chombo kikubwa cha kiintelejensia cha marekani kimekuja juu na kudai kuwa kampuni ya Huawei kwa namna moja au nyingine limepokea fedha kwa ajili ya uwekezaji kutoka kwa mashirika makubwa ambayo kwa namna moja au nyingine yanashirikiana na serekali ya china.

Ni kwamba makampuni ambayo yanatoa fedha hizo moja kwa moja yanajihusisha na mambo ya usalama. Kwa upande wa CIA wameona ni vyema kuyaonya mataifa mengine mengi kama vile Australia, New Zealand na Canada.

Kumbuka kampuni ya Huawei iko mbioni kuingia katika mkataba mkubwa na  Uingereza katika kuhakikisha kuwa Huawei inalisaidia taafa hilo katika kusasisha (Upgradde) teknolojia ya 5G katika mawasiliano.

CIA pia haikuishia hapo ilitaja wafadhili hao ambao ni sehemu ya jeshi (People’s Liberation Army), Tume ya usalama ya China (China’s National Security Commission) na tawi la mtandao wa kiintelejensia wa china (Chinese state intelligence network). Wametaja mashirika haya na kuwaweka wazi watu ambao wanafanya kazi na Huawei na dunia nzima kwa ujumla.

Kwa kifupi ni Kwamba CIA Imewatonya washkaji zake juu ya hili na kuwataka waliangalie kwa kina jambo hili

Kwanini CIA Wamefanya Hivi.

Tukiangazia katika swala zima la ulinzi na usalama, taarifa ndio kitu cha muhimu sana (zinaweza leta/kuvunja usalama). Kwa mataifa makubwa taarifa huwa zinapewa kipaumbele kikubwa na zinatunzwa sana.

Fikiria kama Huawei Kwa mfano akawa kweli kapokea fedha katika makampuni hayo, hii inaonyesha ni moja kwa moja lazima makampuni hayo yataitumia huawei kama chombo chake cha upelelezi na pia kukusanya taarifa za mataifa mbali mbali.

Wanasiasa wengi wamekua na mtazamo tofauti tofauti juu ya jambo hili na wengine wametaka kabisa kampuni hiyo ifungiwe (au ifungiwe kufnaya kazi maeno fulani). Kwa upande wao huawei wamekataa na kusema kuwa hizo ni kashfa tuu kutoka kw CIA ambazo hazina ukweli wowote.

Kwa upande wangu naona hili ni jambo ambalo linaweza kuirudisha huawei nyuma, ikumbukwe kua huawei ina biashara nyingi na mataifa mengi. Hili likibainika kuwa ni kweli basi kampuni itapoteza biashara nyingi.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini mtazamo wako juu ya hili. Kumbuka kutembelea TeknoKona kila siku kwani daima tupo nawe katika Teknolojia!.

Share.

About Author

Leave A Reply