Tuesday, August 20

Dkt Magufuli Kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 21 Februari, 2018 amewasili nchini Uganda ambapo atahudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Ijumaa tarehe 23 Februari, 2018 Mjini Kampala.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe Mhe. Rais Magufuli amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Mhe. Sam Kutesa na kisha kuelekea Ikulu ya Entebbe ambako amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.

Kesho tarehe 22 Februari, 2018 Mhe. Rais Magufuli atahudhuria mkutano maalum katika ngazi ya wakuu wa nchi unaohusu masuala ya miundombinu na afya na keshokutwa tarehe 23 Februari, 2018 na atahudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebe nchini Uganda ambapo pamoja na mambo mengine atahudhuria vikao vya Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki vitakavyoanza kesho jijini Kampala nchini Uganda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.