Monday, June 17

Zitto amkaribisha Maalim Seif, atoa ujumbe kwa Watanzania

0


Dar es Salaam. Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amewakaribisha katika chama hicho waliokuwa wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) akiwamo Maalim Seif Sharif Hamad.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Machi 18, 2019 amesema alichokifanya Maalim Seif si jambo lake peke yake bali ni suala la mapambano ya Wazanzibari na Watanzania katika kudai haki.

“Chama chetu kinawakaribisha wanachama wapya tuendelee na safari ya ukombozi wa kidemokrasia nchini kwetu,” amesema Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Mjini.

Kiongozi huyo wa ACT- Wazalendo ametoa ujumbe kwa Watanzania kuwa, “nawaeleza Watanzania wote kuwa safari ya ujenzi wa demokrasia inaendelea. Mapambano ya kuboresha maisha ya wananchi yanaendelea.”

Zitto amesema nini kuhusu masharti aliyopewa Maalim Seif, kwa nini wamempokea usikose nakala ya gazeti la Mwananchi kesho Jumanne Machi 19, 2019

Share.

About Author

Leave A Reply