Tuesday, August 20

ZFDA yawaonya wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa zinazokaribia kuharibika

0


By Muhammed Khamis, Mwananchi [email protected]

Unguja. Mkuu wa Ukaguzi wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA), Mohd Shadhil amewashauri wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa kutoka nje kuacha tabia ya kununua bidhaa zilizobaki siku chache kuharibika.

Amesema kuna baadhi ya Wafanyabiashara wa Zanzibar huingiza bidhaa zikiwa zimebakiza miezi michache kumaliza muda wa matumizi kwa bei ndogo, wakitegemea kupata faida kubwa wanapoziingiza Zanzibar.

Mkuu wa Ukaguzi wa ZFDA, ameyasema  hayo leo Mei 27, 2019 wakati wakiteketeza zaidi ya tani 183 za bidhaa mbalimbali zilizoharibika na kupitwa na muda wa matumizi kwenye dampo la Kibele, Wilaya ya Kati.

Miongoni mwa bidhaa zilizoteketezwa ni mchele tani 163 ulioingizwa nchini na Kampuni ya Zenj General Marchandize Ltd na unga wa ngano tani sita, ulioharibika baada ya kuingia maji ya mvua.

Huku bidhaa nyingine zikiwa ni tende tani tano, vipodozi tani moja,  juisi na bidhaa mchanganyiko vyote vikiwa vimemaliza muda wa matumizi ya binadamu.

Share.

About Author

Leave A Reply