Monday, August 19

Zari amtambulisha mpenzi wake mpya

0


Kampala,Uganda. Mfanyabiashara wa Uganda na mpenzi wa zamani wa nyota wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platinumz, Zari Hassan ametangaza kwamba amepata mpenzi mpya.

Ni mwaka mmoja sasa na miezi kadhaa tangu alipotangaza kuvunjika kwa uhusiano wake na Diamond.

Mpenzi huyo mpya ambaye amemtaja mpenzi huyo kwa herufi  ‘M’ katika mtandao wake wa Instagram anadai ndiye aliyechukua nafasi ya Diamond.

Akitangaza uhusiano wake mpya katika mtandao huo wa kijamii Zari Hassan alisema kuwa mpenzi wake mpya amemkubali yeye pamoja na watoto wake wote watano.

‘Kwako wewe mpenzi nimejifunza mengi; Nakumbatia maisha yalivyo kwa sababu ya unyenyekevu wako. Nimekuwa nikifikiria maisha yangu ya baadaye lakini sikuweza kujua maisha hayo yatakuwa vipi. Watoto watano, wanaume wengine lakini bado ukaniona mimi kuwa mwanamke mrembo zaidi”, alisema Zari katika chapisho lake lililosomwa na watu  100,000.

”Nakupenda sana bwana M, na sio vitu vyenye thamani unavyonionyesha, nimeviona hivyo na hata vikuu na vizuri zaidi. lakini ni wewe, moyo wako, uwepo wako na vile unavyotufanya mimi na wanangu kukuhisi. Wewe ni jasiri sana bwana M:

Zari alisema yeye mwenyewe ana miaka 38, na ana watoto watano lakini bwana wake huyo umetumwa kutoka mbinguni mpenzi. Nakupenda bwana M,” aliongezea Zari katika chapisho hilo.

Mfanyabiashara huyo wa Uganda alizungumzia kuhusu nafasi yake katika kujenga maisha ya wapenzi wake wa awali ambao anasema hawakumpenda kwa dhati sambamba na kukemea wanaodai kumjua mpenzi wake mpya.

Share.

About Author

Leave A Reply