Monday, August 26

Zahera kuisuka upya Yanga kwa kusajili sita wa kigeni

0


By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Baada ya kuondokewa wa nyota wake wawili Herierit Makambo na Ibrahim Ajibu, kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema atasajili wachezaji nane kati yao sita kigeni na wawili watanzania.

Yanga haijatwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa msimu wa pili mfululizo na imemaliza msimu kwa kuwapoteza nyota wake wawili Ajib amesajiliwa TP Mazembe na Makambo aliyesajiliwa na Horoya AC.

Kocha Zahera alisema wapo pia wachezaji nitakaowaacha msimu huu ambao nitawataja hivi karibuni, lakini nitakaowaongeza ni wanane.

“Tayari wachezaji hao wanane tulishafanya nao mazungumzo kilichobaki ni kusaini mkataba tu.

Alisema kati ya wachezaji hao sita ni wa kigeni na wawili ni wazawa ambao atawaweka wazi baada ya mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu dhidi ya Azam utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wiki ijayo.

“Kila kitu kuhusu usajili wangu msimu huu kimekamilika na hata wachezaji nitakaowaongeza na wale nitakaowaacha, ila wote nitawataja mara tu baada ya mechi yetu na Azam,” alisisitiza.

Alisema hawezi kuweka wazi usajili wake kwa sasa kwani ligi bado haijaisha, hivyo anachosubiri ni kumaliza Ligi kwanza ndipo atangaze usajili wake.


Share.

About Author

Leave A Reply