Friday, August 23

Yanga yatibua mipango ya ubingwa Azam FC

0


By Olipa Assa

KOCHA wa Azam FC, Meja mstaafu wa jeshi, Abdul Mingange amezungumzia kitendo cha kudondosha pointi tatu dhidi ya Yanga kama kinaingiza dosari ya ndoto zake kwa msimu huu.

Mingange anasema kiuhalisia ubingwa kwao umekuwa kwenye mtego mgumu, akikiri Simba na Yanga zinaonekana kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutwaa taji hilo, huku mipango yake ikiwa ni kuhakikisha timu hiyo inamaliza msimu katika nafasi ya pili.

Kocha huyo anafunguka kwamba mahesabu yake yalikuwa kumaliza mechi zilizobakia kwa ushindi, kitendo cha kupoteza na Yanga kimetibua mipango yake.

Baada ya Azam FC jana kupoteza dhidi ya Yanga, imebakiwa na michezo mitano na ikifanikiwa kushinda yote itakuwa na pointi 81 ila kwa sasa ina pointi 66.

“Mfano tungewafunga Yanga, tungemaliza ligi tukiwa na pointi 84, ndio maana nasema kupoteza inatibua mipango yangu, ila kwa sasa hatuna budi kugeukia kwenye kwenye mechi zilizosalia mbele yetu.

“Bado mchezo wa mwisho na Yanga, tunajipanga hatutaki kuwa wateja wao, naamini itwakua mechi ngumu tutakayohitaji kuonyesha kwamba ni washindani na sio mtelemko”alisema.

Yanga imebakiwa na mechi tano, ina pointi 77 ikifanikiwa kushinda yote basi itakuwa inamaliza ligi kwa pointi 92, Simba wao wana pointi 69,wamecheza mechi 27 kabla ya mechi yao ya saa 10:00 jioni na JKT Tanzania, wakishinda mechi 11 walizobaki watamaliza ligi na pointi 102.

Share.

About Author

Leave A Reply