Monday, August 26

Yanga: Ajibu baki nyumbani kumenoga

0


By Charity James

MAKAMU Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema bado wanamuhitaji mshambuliaji wao Ibrahim Ajib kwani wanathamini mchango wake na kama wapinzani wao Simba wametoa kishika uchumba kwa nyota huyo basi wao wapo tayari kutoa mahali.
Ajibu ameingia katika vichwa mbalimbali vya magazeti baada ya kuhusishwa kupata ofa klabu tatu tofauti ikiwemo TP Mazembe na Simba ambao ni waajiri wake wa zamani.
Akizungumza Dar es Salaam  jana, Mwakalebela alisema Ajibu ni mchezaji mzuri na amewasaidia sana msimu ulioisha hivyo wanatambua umuhimu wake kikosini na wanaamini kuendelea kubaki hapo kutakuwa na faida.
“Bado tunaendelea na usajili, wachezaji wote tuliosajili ni mapendekezo ya kocha Mwinyi Zahera na tuna mpango wa kumaliza usajili wetu mapema lengo ni kuingia kambini kujiandaa kwaajili ya msimu mpya wa 2019/20,”
“Tuna mpango wa kuweka kambi nje ya nchi au ndani kubwa tunamsikiliza kocha anataka timu ikaweke kambi wapi, tumejipanga kuandaa kikosi cha ushindani na kuhusua Ajibu namuonya kuwa abaki nyumbani kumenoga,” alisema Mwakalebela.
Aliongeza kuwa wana mpango wa kucheza michezo mitano ya kirafiki ya kimataifa na ya ndani kabla ya msimu mpya haujaanza hiyo itafanyika mara baada ya timu kuingia kambini.


Share.

About Author

Leave A Reply