Sunday, August 25

Wiki ya elimu inasaidia kuongeza ufaulu katika maeneo inakoadhimishwa

0


By Tumaini Msowoya, Mwananchi [email protected] co.tz

Dar es Salaam. Serikali imesema imeandaa utaratibu wa kila Ijumaa kukutana na mashirika ya kiraia yanayojishughulisha na utoaji wa elimu nchini ili kudhibiti yale yanayotumia  changamoto za kielimu kujinufaisha.

Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi anayeshughulikia sekta ya elimu Tixon Nzunda amesema hayo leo Mei 31 wakati akizungumza katika maadhimisho ya juma la elimu yanayoendeshwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET).

Nzunda amesema lengo la Serikali ni kujua shughuli za mashirika hayo na kuyaelekeza kwenye maeneo yenye changamoto ili kusaidia kuzitatua.

“Kila Ijumaa wizara ya elimu inakutana na mashirika yasiyo ya kiserikali kuondoa yale yanayojinufaisha na matatizo ya kielimu na yakipata fedha hayatumii kwa malengo stahiki,” amesema Nzunda.

Amesema wanachotaka ni kujua shughuli zao na  kuyaelekeza mashirika hayo kwenye maeneo yenye changamoto.

“Serikali inafanya mambo yake kwa uwazi kwa hiyo na nyie mashirika tunataka muwe wazi,” amesema Nzunda.

Amesema kila shirika likijenga madarasa matatu maeneo yenye uhaba yatasaidia kupunguza tatizo.

Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) unaundwa na mashirika yasiyo ya kiserikali zaidi ya 180 huku yaliyopo Handeni kwenye maadhimisho hayo yakizidi 20.

Kwa upande wa mwakilishi wa TENMET na Mkurugenzi wa Hakielimu Dk John Kalage amesema lengo lao ni kuibua changamoto na kupanga mikakati ya pamoja ya namna ya kuzitatua.

Amesema kwa zaidi ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwa juma la elimu nchini kumekuwa na mafanikio mengi kwenye wilaya wanazoadhimisha ikiwamo kuongezeka kwa ufaulu.

Amesema tofauti na miaka ya nyuma wakati ambapo huwa wanachagua wilaya ya mwisho kwenye matokeo, safari hii waliamua kuadhimisha Handeni kutokana na ongezeko la ufaulu mwaka hadi mwaka.

Share.

About Author

Leave A Reply