Wednesday, August 21

Waziri wa zamani, raia 4 wauawa katika mlipuko wa bomu Somalia

0Watu wasiopungua 13 walijeruhiwa pia katika mlipuko huo.

Wapiganaji wa kikundi cha al-Shabab wamedai kuhusika na mlipuko huo, wakisema kuwa walikuwa wamekusudia kuwaua wanajeshi, wabunge na maafisa wengine wa serikali.

Al-Shabab mara nyingi wamekuwa wakilipua mabomu katika mji huo mkuu karibu na eneo la ikulu ya rais na katika mahoteli ambayo aghlabu wanafikia maafisa wa serikali na wageni.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.
.

Share.

About Author

Leave A Reply