Wednesday, August 21

Waziri Mkuu wa Papua New Guinea ajiuzulu

0Kupitia taarifa iliyowasilishwa kwa nujia ya barua pepe, O’neill, ambaye amehudumu katika wadhifa wa Waziri Mkuu kwa mika saba, alisema amemkabidhi mamlaka aliyekuwa waziri mkuu wa kisiwa hicho cha bahari ya Pacific ya Kusini, Julius Chan.

O’neill aliongeza kwamba ni matumaini yake hatua hiyo italiwezesha taifa hilo kuuimarisha mchakato ambao umekuwa ukiendelea wa ajenda ya mageuzi ya kisiasa.

Shirika la habari la Reuters liliripoti kwamba misukosuko ya kisiasa ni jambo la kawaida katika kisiwa hicho chenye ukwasi wa raslimali, lakini pia kinachokumbwa na umaskini mkubwa.

Oneill amekuwa akikabiliwa na shinikizo la kuondoka mamlakani kwa muda sasa, kufuatia shutuma mbalimbali, ukiwemo ufisadi.

Umaarufu wake ulionekana kutikisika siku ya Ijumaa wakati wanachama tisa, wakiwemo mawaziri wawili, walipokihama chama kinachotawala.

Share.

About Author

Leave A Reply