Friday, April 19

Wawa hachezi na jukwaa

0


By Doris Maliyaga

PASCAL Wawa kumbe ana madongo bwana! Beki huyo wa kati wa Simba, amesema hafanyi kazi zake kwa kuangalia majukwaa badala yake hutimiza wajibu wake uwanjani na kwamba hana mchecheto na pambano lijalo la watani.

Beki huyo, kwa sasa anacheza nafasi hiyo pamoja na Juuko Murshid raia wa Uganda baada ya Erasto Nyoni kupata majeraha ya goti.

“Kazi yangu ni uwanjani sio kuzungumza na mashabiki, ndio maana sipendi kuzungumza mengi nje ya uwanja kuhusu kazi yangu bali naiacha miguu yangu iongee,” alisema Wawa alioyewahi kuichezea Azam FC na El Merreikh ya Sudan.

Simba ilipofungwa mfululizo mabao 5-0 na AS Vita na Al Ahly ugenini, wadau wengi wa Simba walizungumza juu ya kiwango cha mchezaji huyo, lakini mwenyewe alisema; “Kazi yangu naijua, huwa naifanya uwanjani na si kubishana na mashabiki,” alisema Wawa.

Alisema, wao ni watekelezaji na kuwa wanakwenda kujiandaa, anaamini watafanya vizuri katika mchezo na watani: “Ni mchezo mgumu lakini si mara ya kwanza, tumejiandaa na tunakwenda kwa maandalizi mengine zaidi.”

Simba na Yanga zitavaana keshokutwa Februari 16 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ni wa mzunguko wa pili.

Share.

About Author

Leave A Reply