Tuesday, August 20

Wanga atemwa kikosi cha Harambee Stars

0


By Fadhili Athumani

Nairobi. Kinara wa mabao katika msimu uliomalizika wa Ligi Kuu Kenya, Allan Wetende Wanga ametemwa katika kikosi cha wachezaji 27, wa timu ya Taifa Kenya kitakachoondoka Jumamosi hii, kuelekea Ufaransa kwa ajili ya kambi ya wiki tatu, kujiandaa na fainali za michuano ya mataifa ya bara la Afrika, AFCON 2019.

Allan Wanga ameongoza za mbio kuwania kiatu cha dhahabu akiwa na mabao 18, huku mpinzani wake akiwa ni Enosh Ochieng mwenye mabao 17, lakini akiwa amesalia na mechi moja, amekuwa ni mmoja wa nyota watatu waliotemwa na Mfaransa Sebastien Migne.

Wengine walikuwa katika kikosi cha awali cha wachezaji 30, lakini wakapitiwa na panga la Mfaransa huyo ni pamoja na Kipa namba mbili wa Kariobangi Sharks, Brian Bwire na kiungo wa AFC Leopards, Whyvonne Isuza.

Wachezaji waliojumuishwa katika kikosi hicho cha wachezaji 27 ni ingizo jipya Christopher Mbamba, Cliff Miheso, Joseph Okumu na John Avire, ambaye amepandishwa kutoka kikosi cha U23 kuchukua nafasi ya Wanga.

Stars imerudi katika michuano hiyo baada ya miaka 15, imepangwa katika Kundi C, pamoja na majirani zao Tanzania, Senegal na Algeria. Ikiwa kambini, Stars itajipima nguvu na Madagascar (Juni 7) na DR Congo (Juni 15) kabla ya kuelekea Misri (Juni 19).

Kikosi cha Harambee Stars;

Makipa: Patrick Matasi, John Oyemba, Faruk Shikalo

Mabeki: Abud Omar, Joash Onyango, Joseph Okumu, Musa Mohammed, David Owino, Bernard Ochieng, Brian Mandela, Philemon Otieno, Eric Ouma

Viungo: Victor Wanyama, Anthony Akumu, Ismael Gonzalez, Ayub Timbe, Francis Kahata, Ovella Ochieng, Dennis Odhiambo, Eric Johanna, Paul Were, Cliffton Miheso, Johanna Omollo

Mastraika: John Avire, Masud Juma, Christopher Mbamba, Michael Olunga


Share.

About Author

Leave A Reply