Tuesday, March 19

Wanafunzi wafariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta

0


By Aurea Simtowe, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Wanafunzi  wa shule  za Msingi Kijichi na Bwawani zilizopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Nasri Mustapha na Sabra Salum  wamefariki dunia baada ya kuangukia na ukuta.

Tukio hilo limetokea leo Alhamisi Desemba 6, 2018 wilayani humo wakati wanafunzi hao wa darasa la kwanza na la pili wakicheza karibu na ukuta huo uliozunguka shule hizo.

Akizungumza na Mwananchi leo Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Temeke, Emmanuel Lukula amesema, “Majeruhi wawili ambao ni Sharifa Jumanne na Mukrini Stambul tuliwapeleka hospitali ya wilaya ya Rangitatu na Rehema Nongwa tulimpeleka hospitali ya Rufaa ya Temeke kutokana na hali yake.”

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Temeke.

Share.

About Author

Leave A Reply