Saturday, August 17

Wanafunzi wa Florida wanaandaa maandamano DC na kwingineko

0
Wanafunzi walionusurika na mauwaji katika shule ya sekondari Marjory Stoneman Douglas huko Florida nchini Marekani wametangaza maandamano mjini Washington  na miji mingine muhimu ya Marekani  mwezi ujao  ili kudai hatua thabiti zaidi zichukuliwa kuzuia mauwaji mengine kuweza kutokea katika shule za nchini Marekani.

Cameroon Kasey mwanafunzi wa shule ya sekondari alikiambia kipindi cha “This week” cha kituo cha televisheni cha ABC kwamba “tutaandamana pamoja kama wanafunzi ili kuwa aibisha wanasiasa  wanaokubali kupokea fedha kutoka chama cha wamiliki bunduki Marekani-NRA. Na tutataka maisha yetu yalindwe.”

Alizsema NRA inahamasisha mila ya umiliki bunduki  inayosababisha maafa haya yote.

Mwanafunzi mwingine Emma Gonzalez ameiambia ABC kwamba Rais Trump, Seneta Marco Rubio wa jimbo la Florida na gavana wa jimbo lao Rick Scott wanaunga mkono NRA.Gonzalez alisema hawatakwenda katika kikao cha Rais Trump  siku ya Jumatano.

White House imetangaza kwamba Rais Trump atakutana na wanafunzi pamoja na walimu wao katika kikao cha kusikiliza madai yao  lakini White House haikutoa maelezo zaidi juu ya kikao hicho.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.