Sunday, August 25

Wametisha Ligi Kuu Bara, lakini hawaendi Misri

0


By Matereka Jalilu

Dodoma. Achana kabisa na wachezaji 39 walioitwa na kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars, Emmanuel Amunike ambao watachujwa na kubaki 23 watakaokwenda Misri kuwakilisha Tanzania katika fainali za Mataifa Afrika {Afcon} mwaka huu.

Wachezaji wengi walifanya vema msimu huu wa ligi uliomalizika, lakini hawapata nafasi ya kujumuishwa katika kikosi cha awali cha Amunike.

Tovuti ya Mwanaspoti kama kawaida linakuletea baadhi ya wachezaji waliong’ara, lakini hawajaitwa na hata wangeitwa bado kusingekuwa na mshangao wowote ule kutokana na jinsi walivyotisha msimu huu.

Paulo Godfrey ‘Boxer’

Kuumia na kutokuwa fiti kwa Juma Abdul msimu huu kulimpa nafasi kinda huyo kutumia vema nafasi hiyo adhwimu na kuonyesha makeke yake akibebwa zaidi na kasi wakati wa kukaba na kushambulia jambo lililomfanya ajihakikishie namba katika kikosi cha kwanza hata aliporejea mwenye namba yake Juma Abdul.

Ni bahati mbaya kwake tu uwepo wa Shomari Kapombe na Hassan Kessy kumemfanya asiwe na nafasi ya kujumuishwa katika kikosi cha Stars katika maandalizi ya kwenda Misri.

Abdallah Shaibu ‘Ninja’

Beki mwingine wa Yanga alikabidhiwa jukumu la kurithi mikoba ya aliyekuwa beki wao na nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Canavaro’ ambapo kukabidhiwa huko ikiwemo namba ya jezi kulipelekea Shaibu kujiamini zaidi.

Ninja amekuwa na uhakika wa namba msimu huu akicheza kwa nyakati tofauti na mmoja wapo kati ya Vincent Andrew au Kelvin Yondani na wakati mwingine akitumika kama kiungo wa ulinzi {namba 6} katika mechi ambazo walicheza kwa lengo la kukaba zaidi hususani mechi dhidi ya Simba.

Salum Abubakar ‘Sure Boy’

Kuachwa kwake katika kikosi cha Stars kulizua gumzo ni kiungo huyu fundi anayechezesha kwa ustadi mkubwa katika timu yake Azam, lakini ni bahati mbaya kwake ameachwa katika kikosi cha awali cha kocha Amunike.

Sure Boy alikuwa anajumuishwa katika baadhi ya mechi za kusaka tiketi, lakini katika mechi za mwisho ikiwemo dhidi ya Uganda alitemwa na hata kikosi cha mwisho amekosekana.

Kiungo huyu wa mabingwa mfululizo wa ligi kuu bara Simba, Hassan Dilunga naye hajajumuishwa katika kikosi cha awali Stars, licha ya kuwa na msimu bora katika klabu yake ikiwemo katika mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Dilunga mbali na kuachwa katika kikosi cha awali pia hakuwa na bahati ya kujumuishwa mara kwa mara katika kikosi cha Stars katika mechi za kufuzu licha ya kwamba hata angeitwa isingeshangaza kulingana na ubora wake ulivyo.

Kiungo mshambuliaji wa Alliance, Ambundo amekuwa na msimu bora kabisa katika Ligi Kuu baada ya kufanikiwa kufunga mabao 10 msimu huu.

Ambundo naye hajakutana na ‘zali’ la kujumuishwa katika kikosi cha awali cha Amunike licha ya kutisha msimu huu.

Pale Azam kuna huyu kiungo ambaye ametumika kwenye mbinu tofauti za makocha wote Hans Pluijm kabla ya kufukuzwa na Meja Abdul Mingange aliyemalizia msimu kwa pamoja wamemtumia vema winga huyu naye hajawaangusha.

Mahundi amekuwa na mwendelezo bora msimu huu akiing’arisha Azam na kufanikiwa kuaminiwa mbele ya viungo wengine Enock Atta Agyey na Ramadhan Singano lakini hiyo haikuwa sababu kwa kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike kumjumuisha katika kikosi chake.

Mshambuliaji wa Mwadui ni gumzo kila ilipotajwa orodha ya wachezaji wa Stars bila uwepo wa jina lake ambapo baadhi ya waliishia kushangaa na kuhoji kwamba inakuwaje mchezaji aliyepo kwenye vita ya ufungaji bora haitwi kwenye kikosi hicho cha Amunike ikiwemo kikosi cha awali wachezaji 39 wanaojiandaa na fainali hiyo nchini Misri.

Straika mwingine aliyefanya vema msimu huu ni Jafary Kibaya wa Mtibwa Sugar hana cha kuuliza wala kuhoji kutoitwa kwake Taifa Stars kutokana na ukweli kwamba timu hiyo imesheheni washambuliaji bora wanaocheza nje ya nchi kama vile Samatta, Rashid Mandawa, Shaban Idd, Adi Yusuph, Thomas Ulimwengu na wanaocheza nchini akiwemo John Bocco.

Kama ilivyo kwa Kibaya, ndivyo ilivyo kwa mshambuliaji wa Mbao ya Mwanza naye amekuwa na msimu mzuri ambao ungeweza kumfanya aitwe na kocha Emmanuel Amunike na isiwe ajabu kulingana na alivyong’ara lakini uwepo wa washambuliaji wengi hana ujanja.


Share.

About Author

Leave A Reply