Monday, June 17

Wakitua tu , heshima ya Old Trafford inarudishwa upyaa bana

0


SIO siri msimu wa 2018/19, umekuwa moja ya misimu mibaya zaidi kwa Manchester United kwenye Ligi Kuu England. Walipoteza mechi nane katika michezo 12 ya mwisho ukiwemo ule wa kufunga pazia la msimu.

Mashetani wekundu walipokea ubatizo wa moto kutoka kwa Barcelona (3-0), katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya. Wakapigwa na Everton (4-0), kabla ya kupokea kichapo cha 2-0, kutoka kwa vibonde Cardif City, walioshuka daraja.

Tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson, United hawajatwaa ubingwa wa EPL hata mara moja, licha ya kusajili mastaa kadhaa kama, Paul Pogba, Alexis Sanchez, Angel Di Maria na Romelu Lukaku. Mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2013.

Ukiachana na ubutu wa safu ya ushambuliaji, Man United pia imekuwa na tatizo katika safu yao ya kiungo na beki. Msimu ujao, endapo Ole Gunnar Solskjaer, atawapata nyota hawa watano, watamsaidia kurudisha heshima pale Old Trafford.

Kumekuwa na tetesi nyingi kuwa, Muargentina huyu, yuko njiani kuihama Juventus. Wakala wake, ambaye ni kaka yake, Gustavo Dybala, hivi karibuni alinukuliwa akisema staa huyo, hana furaha kabisa pale Turin.

Mshambuliaji huyu wa zamani wa Palermo, huenda akapata amani baada ya kuondoka kwa Massimiliano Allegri, ambaye hakuwa na mzuka naye kabisa, lakini United bado wanaweza tumia mwanya wa matatizo yake uwanjani, kupata saini yake.

Kiwango cha Dybala, kim kuwa kikiporomoka kila uchao, tangu Cristiano Ronaldo alipotua Turin. Msimu uliomalizika amefunga mabao matano tu, tofauti na msimu uliopita ambao alifunga mabao 22. Vita vya mafahali wawili, vinamkimbiza Turin.

Kutokana na staili yake akitua Old Trafford basi ni mzuka sana kwani, hauna tofauti na uchezaji wa Lionel Messi na itakuwa ni rahisi kuwa staa na kumfunika Lukaku. Uhusiano wake mzuri na Paul Pogba, utaisaidia sana Man United kurejesha heshima yake.

Aidha, Dybala sio mchoyo. Hii itaongeza kasi ya ushambuliaji ya United, ambayo tayari inajivunia uwepo wa Marcus Rashford na Anthony Martial. Hebu piga picha itakuwaje kama Man United ikiwasimamisha Dybala, Rashford na Martial pale mbele?

Kinda huyu wa Uingereza, amekuwa sehemu ya ngome isiyopitika ya klabu ya Crystal Palace. Ni mmoja wa wachezaji walioisaidia, kufanya vizuri msimu huu. Aaron Wan-Bissaka, anatajwa miongoni mwa mabeki bora waliopo kwenye ligi tano kali za Ulaya.

Rekodi inaonesha kuwa, ana wastani 3.7 wa kupokonya mipira, wastani wa kuzuia mipira 2.4 na 3.7 ya kuondoa hatari. Pia ni mzuri hewani, ambapo ana wastani wa 1.2 ya kushida mipira ya juu, jambo linalochangiwa na urefu wake.

Mbali na ubabe wake katika safu ulinzi, Wan-Bissaka ana rekodi nzuri ya kupandisha mashambulizi, ambapo ana asisti tatu. Ukiangalia beki ya United, kwenye msimu wa 2018/19, utaona wameruhusu mabao mengi sana msimu.

Ujio wa Wan Bissaka, utawaongezea nguvu kina Ashley Young, Phil Jones na Chris Smalling, pale nyuma. Huyu ataisaidia kikosi kuwa huru zaidi, lakini atamkinga David de Gea, kutokana na dhoruba kali pale langoni.

Kila mtu ameshuhudia namna ambavyo Liverpool, walimwaga fedha nyingi kuipata huduma ya mchezaji bora wa EPL, msimu wa 2018/19, Virgil van Dijk, ambaye kwa kiasi kikubwa ameifanya Liverpool, kuwa moja ya klabu bora Ulaya.

Man United wanaweza kuwaiga Liverpool, kwa kumsajili nahodha na beki wa Ajax, Matthijs de Ligt.

Kinda huyu wa Uholanzi, ana uwezo mzuri wa

kukaba, kushambulia na kuongoza jahazi uwanjani. Ni mfungaji mzuri, lakini pia ni mfia timu.

Msimu huu, ameiongoza Ajax kutwaa ubingwa wao wa 34 katika Ligi Kuu ya Uholanzi, baada ya miaka sita, na ubingwa wa KNVB Beker, huku pia wakifika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kishindo, wakiwabwaga mabingwa watetezi Real Madrid na Juventus.

Matthijs de Ligt (19), ni mzuri katika mipira ya juu, na anaweza tengeneza kombinesheni nzuri na Phil Jones na Chris Smalling, kama sio kuziba pengo lao. Anahusishwa pia na Barcelona, lakini hakuna dili iliyosainiwa, hivyo United wana nafasi kama itaamua kumfuata.

Nyota ya Jadon Sancho, imeendelea kung’aa tangu alipojiunga na Borussia Dortmund, akitokea Manchester City, mwaka 2017. Uhamisho huo, ulimshuhudia kinda huyu wa Uingereza akibadilika kutoka mchezaji wa kawaida, hadi mmoja wa mastaa wanaowindwa zaidi duniani.

Thamani yake pia imepanda maradufu. Hivi sasa, kumpata Sancho (19), lazima uwe tayari kulipa Euro 100 milioni. Msimu huu, amefunga mabao 11, na kuongoza kwa asisti, kwenye Bundesliga. Kwa muda mrefu amekuwa akihusisha na mashetani wekundu.

Tangu achukue mikoba ya ukocha pale Old Trafford, Ole Gunnar Solskjaer, amekuwa akihangaika kupata winga tegemeo, kwenye kikosi chake bila mafanikio. Juhudi za kuwajaribu Jese Lingard, Martial, Juan Mata, na Alexis Sanchez, katika nafasi hazijazaa matunda.

Martial na Rashford, ni aina ya mawinga wanaopenda kufunga kuliko kutoa krosi za mabao. Hapa ndipo ubutu wa Lukaku unapoanzia. Ujio wa Sancho unaweza kuwa tiba sahihi kabisa kwa Lukaku.

Kiungo huyu, raia wa Hispania, hakuweza kupata namba ya kudumu katika kikosi cha Barcelona, licha ya kuwa zao la akademi yao ya La Masia.

Alianza katika mechi 15 za msimu mzima wa 2012/13. Hata hivyo, Pep Guardiola, alipompeleka Bayern Munich (2013), aliionesha dunia nzima, uwezo wa miguu yake. Alianza kwa kasi ya kusuasua pale Allianz Arena, lakini kwa sasa, kila kitu kimebadilika.

Amekuwa Staa katikati ya kundi la wajerumani. Alcantara ni aina ya kiungo, ambaye Solskjaer anamtafuta. Ni injini yenye uwezo wa kupiga pasi, kupiga chenga, kufunga mabao na wakati huo huo, akakaba mpaka kivuli cha wapinzani. Ni mrithi sahihi wa kiatu cha Ander Herrera, aliyeondoka Old Trafford.


Share.

About Author

Leave A Reply