Saturday, August 24

Vijana watakiwa kuchangamkia fursa za ujasiriamali

0


By Beldina Nyakeke Mwananchi [email protected]

Musoma. Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Mzee  Mkongea amewataka vijana kuacha kulalamika kuhusu ukosefu wa ajira, badala yake watumie fursa zilizopo kujiajiri ikiwamo asilimia 10 ya mikopo ya Halmashauri inayotolewa kwa ajili yao.

Mkongea amesema kumekuwepo na tabia kwa baadhi ya vijana kushinda vijiweni kwa madai ya kukosa ajira huku wengine wakitumbukia katika matumizi ya madawa ya kulevya hivyo kuwataka kuacha mara moja, badala yake kutumia fedha hizo kwa ujasiriamali.

Akizungumza katika Kijiji cha Kurwaki, Halmashauri ya wilaya ya Musoma vijijini leo Mei 31, 2019 wakati alipotembelea  kikundi cha vijana kilichonufaika na mikopo ya Halmashauri,   amesema Serikali haiwezi kuajiri watu wote kwa wakati mmoja.

Amesema kwa kulitambua hilo   ndio maana imeamua kutenga kiasi cha asilimia 10 ya mapato ya halmashauri kwa ajili ya mikopo ya vijana, hivyo wakiitumia vizuri itawasaidia kujiajiri na kuajiri wengine.

Kwa upande wa kijana Mjenga Nyamarwa amesema kuwa umefika muda sasa vijana wajiunge katika vikundi ili iwe rahisi kupatiwa  mikopo kwa ajili ya kuanzisha shughuli za uzalishaji.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya hiyo John Kayombo amesema kuwa hadi  sasa  Halmashauri yake imekwishatoa asilimia 96 ya mikopo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

“Mbali ya kutoa mikopo hiyo, pia tunatoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana wanaopewa  ili wazitumie fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa, ”amesema Kayombo.

Mwenge wa Uhuru uko katika halmashauri ya  Wilaya ya Musoma vijijini na unatarajiwa kukakua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi sita yenye thamani ya zaidi ya Sh3 bilioni.

Share.

About Author

Leave A Reply