Friday, July 19

VIDEO: Mbowe, Matiko wavuka kihunzi cha kwanza dhamana yao

0


By James Magai, Mwananchi [email protected]

Dar. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mhazini wa Baraza la Wanawake wa chama hicho (Bavicha) Esther Matiko wamevuka kikwazo cha kwanza cha rufaa ya dhamana yao baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kukubali kusikiliza rufaa hiyo.

Wamevuka kihunzi cha pingamizi la Serikali baada ya Mahakama kutupilia mbali hoja za pingamizi hilo.

 Mbowe na Matiko ambaye ni mbunge wa Tarime mjini, wamekata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana katika kesi ya jinai inayowakabili lakini Serikali iliwasilisha pingamizi la awali ikitoa sababu tatu za kutaka rufaa hiyo itupwe pamoja na mambo mengine ikidai rufaa hiyo iko mahakamani isivyo halali kwani inakiuka vifungu vya sheria.

Katika uamuzi wake leo Ijumaa Novemba 30, 2018 Jaji Sam Rumanyika amekataa sababu ya pingamizi la Serikali kuwa liko mahakamani isivyo halali.

Jaji Rumanyika amesema rufaa hiyo iko mahakamani kihalali kwani si lazima kutaja kifungu cha kisheria kinachochapishwa ambao inasomeka vizuri.

Pia Jaji Rumanyika amekubaliana na hoja ya pingamizi la Serikali  sababu mbili za rufaa za kupinga masharti ya dhamana zinakiuka matakwa ya sheria kwa kuwa zimekatiwa rufaa bila kutoa kwanza taarifa ya kusudio la kukata rufaa kupinga masharti hayo ya dhamana yaliyotolewa kati ya Machi na April.

Hivyo Jaji Rumanyika amepanga kusikiliza rufaa hiyo saa nane mchana huu.

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kitakachojiri mahakamani hapo

Soma zaidi : Rufani ya Mbowe ikiendelea mahakamani, Polisi wawatawanya wafuasi wa Chadema

 

Share.

About Author

Leave A Reply