Tuesday, August 20

VIDEO: Emery kupiga panga vichwa kibao Arsenal

0


ARSENAL inajiandaa kupitisha panga kali kufyeka vichwa vya ovyo kwenye kikosi chao mwishoni mwa msimu huu baada ya kocha Unai Emery kuchoshwa na wachezaji wa ovyo ovyo waliopo kwenye timu hiyo.

Beki, Shkodran Mustafi ametajwa kuwa ni mmoja ambaye atafunguliwa mlango wa kutokea licha ya kwamba alinaswa kwa pesa nyingi, Pauni 35 milioni mwaka 2016.

Mjerumani anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye kikosi hicho, Mesut Ozil naye atafunguliwa mlango wa kutokea ili kuondoa bajeti ya Pauni 350,000 kwa wiki wanayomlipa kiungo huyo mchezeshaji. Panga hilo limedaiwa huenda likampitia pia Henrikh Mkhitaryan, anayelipwa Pauni 180,000 kwa wiki ili kufungua milango kwa Kocha Emery kufanya usajili wa wachezaji wengine watakaokuja kuleta maana kubwa katika kikosi.

Hata hivyo, hao si wachezaji pekee ambao Arsenal inasubiri tu ofa ya kuwapiga bei, bali wengine ni Calum Chambers, Mohamed Elneny, Carl Jenkinson na David Ospina huku Danny Welbeck ikielezwa hatapewa mkataba mpya wakati Aaron Ramsey na Petr Cech imeshafahamika wazi kwamba wataachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Mchezaji Denis Suarez aliyebebwa kwa mkopo ataruhusiwa kurudi kwenye timu yake ya Barcelona ili kocha wa timu hiyo kufanya vyema kwenye bajeti yake ya kufanya usajili. Emery anahitaji kuuza ili kuboroesha mfuko wake wa usajili ambapo kwa sasa amedaiwa atakuwa na Pauni 45 milioni tu za kufanya hivyo.

Share.

About Author

Leave A Reply