Thursday, February 21

Vibonde Mwadui, Alliance na African Lyon kazi kwao

0


Dar es Salaam. Timu za Mwadui FC, Alliance FC na African Lyon ndiyo kama vibonde kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara kutokana na namna wanavyopishana mkiani.

Mwadui FC iliyocheza mechi 10, na iko mkiani kabisa kwenye msimamo wa ligi wenye timu 20, itaikaribisha Lipuli FC ya Iringa iliyo nafasi ya 14, kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.

Timu hiyo inayotoka kwenye migodi ya dhahabu inatakiwa kufanya kila wawezalo ili waibuke na ushindi.

Timu nyingine ya Alliance FC nao wana majanga hao. Watakuwa nyumbani kucheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza lakini   tangu waanze kunolewa na Kocha Dady Gilbert baada ya Mbwana Makata kufutwa kazi.

Ilijikongoja kwa Singida United mchezo uliopita na kuvuna pointi tatu ambazo zimewaweka nafasi ya pili kutoka mkiani na pointi 7, kama wataifunga Mtibwa Sugar watazidi kujiimarisha katika nafasi nzuri zaidi. Mtibwa wao ni miongoni mwa timu zinazoutafuta usukani wa kuongoza ligi, wako nafasi ya 4, na pointi 23.

Kibonde mwingine ni African Lyon ambao wanashika nafasi ya tatu kutoka mkiani wakiwa na pointi 7, wiki hii wao watakuwa kwenye mapumziko baada ya mchezo wao na Yanga kusogezwa mbele wakipisha mechi ya Taifa Stars.

Share.

About Author

Leave A Reply