Saturday, August 24

Van Persie ataja vichwa vyake matata

0


LONDON, ENGLAND.STAA Robin van Persie amewataja wachezaji sita anaowaamini ni bora ambao amecheza nao wakiwamo wakali wanne wa Manchester United.
Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal, ambaye alitumikia misimu yake mitatu ya mwisho England kwenye kikosi cha Manchester United huko Old Trafford, amestaafu soka akiwa na umri wa miaka 35.
Van Persie alijiunga na Man United kwa uhamisho wa utata mwaka 2012 baada ya kugomea kusaini mkataba mpya huko Arsenal. Lakini, baada ya kutua tu Man United, ameshinda ubingwa wa Ligi Kuu England katika msimu wake wa kwanza tu huko Old Trafford.
Na straika huyo wa Kidachi annaonekana kukumbuka zaidi maisha yake alipokuwa Man United baada ya kuwataja wachezaji wanne wa kutoka katika timu hiyo kwenye orodha ya wakali wake sita bora aliowahi kucheza nao timu moja.
Van Persie alipoulizwa amtaje mchezaji mchezaji mmoja mwenye kipaji zaidi, alisema: “Ni ngumu kumtaja mmoja. Nitawachagua Dennis Bergkamp, Thierry Henry, Ryan Giggs, Paul Scholes, Wayne Rooney na Ruud van Nistelrooy.”
Van Nisterlooy aliondoka Old Trafford mwaka 2006, muda mrefu sana kabla hata Van Persie hajatua Man United, huku fowadi huyo akiwataja Nemanja Vidic na Rio Ferdinand ni mabeki wagumu zaidi aliowahi kukamiliana nao.
Baada ya miaka mitatu ya kukipiga Fenerbahce, Van Persie alirudi kwao Uholanzi katika mwaka wa mwisho wa maisha yake ya soka kama mchezaji akikipiga Feyenoord.


Share.

About Author

Leave A Reply