Saturday, August 24

Utouh ‘alibip’ Bunge, adai halisimamii mapendekezo ya CAG

0


By Elias Msuya, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Ludovock Utouh amesema Bunge limeshindwa kusimamia mapendekezo ya ripoti za CAG kwa Serikali huku akimtetea Profesa Mussa Assad aliyepishana kauli na chombo hicho cha kutunga sheria hivi karibuni.

Mbali na Bunge, Utouh ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwajibikaji wa Umma (Wajibu), amewakosoa baadhi ya mawaziri aliosema wamekimbilia kujibu mapigo ya ripoti ya CAG kwa kuwa hawahusiki.

Akizungumzia kauli za Utouh, Spika wa Bunge, Job Ndugai licha ya kukataa kutoa maoni, alihoji kwa nini Utouh asipeleke maoni hayo Bungeni.

Utouh ameyasema hayo leo wakati wa uwasilishaji wa uchambuzi wa ripoti za CAG za miaka mitatu, jijini Dar es Salaam.

“Katika umri wangu huu sijawahi kusikia mambo haya popote duniani, lakini sasa nayasikia Tanzania. Msuguano kati ya Spika na CAG. CAG spoke (alizungumza) Bunge ni dhaifu. Anaiagiza Serikali na Bunge linatakiwa lisimamie, tumeona hapa takwimu, is that strong (Je, lina nguvu)?” amehoji Utouh.

Awali, akiwasilisha uchambuzi wa ripoti tano za ufanisi za CAG, ofisa wa Wajibu, Andendekisye Mwakabula amesema zilikiwa na mapendekezo 85 kwa taasisi 10, lakini yaliyotekelezwa ni asilimia 26 tu.

Kuhusu mawaziri kujibu ripoti za CAG, Utouh aliendelea kusema, “mawaziri wanapanguaje hoja za CAG? Kwa sababu zile siyo siasa, inaeleza kabisa nani anahusika.”

Share.

About Author

Leave A Reply