Monday, August 26

Utalii wa utamaduni washika kasi Japan

0


By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Wakati Tanzania ikiimarisha miundombinu ya kufika kwenye hifadhi za Taifa na mbuga za wanyama nchini Japan, juhudi zinaongezwa kuimarisha utalii wa utamaduni.

Ripoti ya Shirika la Kimataifa la Utalii (UNWTO) iliyotolewa leo Jumatatu Mei 27, 2019, inaonyesha asilimia 42 ya manispaa nchini humo tayari zimeandaa vituo vya utalii huo na asilimia 38 ya wilaya zinapanga kufanya hivyo siku za karibuni.

“Kadiri watalii wanavyohangaika kutafuta vivutio tofauti kwenye jamii mbalimbali, ndivyo utalii wa kiutamaduni unavyoshika kasi na kuchangia kufanikisha Malengo Endelevu (SDG) ya Umoja wa Mataifa,” amesema  Zurab Pololikashvili, katibu mkuu wa UNWTO.

Ingawa aina hiyo ya utalii ni mpya nchini Japan, kasi ya ukuaji wake ripoti hiyo inasema ni kubwa katika miaka ya hivi karibuni na unachangia kwa kiasi kikubwa kuchangamsha uchumi wake na unawashirikisha wananchi wengi zaidi.

“Kwa mifano iliyopo Japan, ripoti hii inadhihirisha jinsi Taifa hilo lilivyojipanga kunufaika na aina hii ya utalii ambayo ni nyenzo muhimu ya maendeleo, ushirikishaji wananchi na muungano wa kikanda,” amesema Pololikashvili.

Utalii ni miongoni mwa sekta zinazoongoza kwa kuchangia uchumi wa mataifa mbalimbali duniani ikiwamo Tanzania inayotajwa kuwa ya pili kwa wingi wa vivutio duniani ikizidiwa na Brazili pekee.

Kwa mwaka ulioishia Machi 2019, ripoti ya kila mwezi ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaonyesha thamani ya usafirishaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi iliongezeka hadi Dola 8.54 bilioni za Marekani kutoka Dola 8.48 bilioni zilizoingia kwa mwaka ulioishia Machi 2018.

Asilimia 47.8 ya mauzo hayo yametokana na huduma hasa utalii na usafirishaji ambazo mapato yake yaliongezeka kutoka Dola 3.82 bilioni mwaka 2018 hadi Dola 4.08 bilioni mwaka 2019.

Sekta ya utalii kwa mwaka huo, ripoti inasema ilikua kwa asilimia 13.2 na kufikisha Dola 2.52 bilioni kutokana na ongezeko la wageni walioingia nchini.

Katika juhudi za kukuza utalii, hatua kadhaa zimechukuliwa na Serikali ndani ya miaka michache iliyopita ikiwamo kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) pamoja na kuimarisha barabara za kwenda kwenye vivutio hasa mbuga wa wanyama na hifadhi za Taifa.

Kama ilivyo Japan na mataifa mengine yaliyoendelea, Tanzania inahamasisha utalii wa kiutamaduni unaohusisha vyakula na vinywaji vya kienyeji vinavyopatikana kwenye jamii husika.

Kuongezea, jamii zinahamasishwa kuendeleza ngoma na utamaduni walionao ili kuwapa uzoefu tofauti wageni wanaokuja kujifunza mambo tofauti nchini.

Matunda ya juhudi hizo zote, yameanza kujitokeza baada ya Waisrael 1,000 na zaidi ya Wachina 340 kutembelea vivutio vilivyopo nchini hivi karibuni.

Share.

About Author

Leave A Reply