Friday, July 19

USHAURI WA DAKTARI: Watoto wanaozaliwa na baba mwenye umri mkubwa na matatizo ya ‘afya ya akili’

0


“Tunapozungumzia masuala ya uzazi, mwanaume hazeeki.” Watu wengi hupenda kutumia msemo huu. Lakini hata kiafya pia kuna asilimia nyingi za ukweli zinazopatikana katika msemo huu.

Kwa maana rahisi mwanamume anakuwa na uwezo wa kutungisha mimba hata kama akiwa kwenye umri wa uzee, tofauti na mwanamke ambae kadri anapo ukaribia utu uzima, ndipo anapoanza kupoteza uwezo wa kushika ujauzito kutokana na sababu za kiumri ambazo zinaenda kuathiri utendaji kazi wa mfumo wake wa vichocheo na mfumo wa uzazi kwa ujumla.

Wanawake wengi huanza kupoteza uwezo wa kuzaa kuanzia umri wa miaka 40 hadi 50 na kuendelea, japo kuna wanawake wachache ambao hufanikiwa kushika ujauzito katikati ya umri wa miaka 40 hadi 50.

Lakini kwa mwanaume, hali ni tofauti, kwani anaweza akawa na uwezo wa kutungisha mimba hata akiwa na miaka 60.

Kwenye jamii zetu kumekuwa na mitazamo tofauti tofauti tunapokuja kwenye suala la wazazi kupata watoto kwenye umri mkubwa zaidi yaani kuanzia miaka 40, 45 na kuendelea, kuhusiana na faida na hasara zake kwa wazazi hata mtoto wanae mzaa pia.

Wengi husema kuwa mtoto anayezaliwa na wazazi ambao umri wao aidha mzazi mmoja au wote kiumri wanakaribia uzee, huwa na akili nyingi na hasa za darasani. Lakini pia wengine husema kuwa watoto hawa wanaozaliwa na wazazi ambao kiumri umeenda huwa wazembe na wazito kiakili.

Haya ni mawazo na mitazamo tofauti tofauti ambayo kila mmoja anayo kuhusiana na jambo hili. Lakini je, kisayansi hii ipoje? Kuna madhara yeyote ya kuzaa katika umri mkubwa ambayo mzazi anaweza kukutana nayo, na mtoto pia anaweza kuyapata? Kama yapo ni yapi?

Kwanza kabisa ifahamike kuwa, kiafya si vizuri sana kuzaa katika umri mkubwa kwa sababu jambo huhatarisha afya ya mzazi mwenyewe na mtoto.

Madhara kwa upande wa mzazi humpata mama pekee kwa asilimia nyingi, lakini madhara ya upande wa mtoto anaweza akazaliwa nayo na yakadumu hadi ukubwani.

Kwanza kabisa tunapozungumzia madhara ya kiafya kwa mtoto, kuzaa katika umri ulioenda kuna uhusiano mkubwa na kupata mtoto mwenye usonji au (autism). Tafiti mbalimbali za kisayansi zimethibitisha kuwa, wazazi ambao umri wao umeenda na hasa baba, wapo hatarini sana kupata mtoto mwenye usonji.

Tafiti zinaonesha kuwa, uhusiano kati ya mama mwenye umri mkubwa na mtoto mwenye usonji ni mdogo sana ukilinganisha kwa upande wa baba. Baadhi ya watoto wamekuwa wakizaliwa na tatizo hili la usonji kutokana na wazazi wao wa kiume kuwa na umri mkubwa.

Hapa ndipo tunaporudi kwenye zile dhana zilizopo vichwani mwa watu wengi kwenye jamii zetu kuwa, kuzaa mtoto kwenye umri mkubwa kunasababisha kupata watoto wenye matatizo ya akili. Huenda usemi huu una ukweli kwenye dhana ya kiafya.

Share.

About Author

Leave A Reply