Wednesday, August 21

Unataka kushuka daraja msajili Kapera

0


By Charity James

Dar es Salaam. Wakati kiungo wa Stand United, Jacob Masawe akiwa na rekodi ya kuzisaidia baadhi ya timu alizocheza zisishuke daraja ni tofauti kwa mshambuliaji Ramadhani Kapera ameonekana anagundu kwani kila timu ya Ligi Kuu aliyopitia inashuka daraja.

Kapera anahusishwa kukipiga Simba msimu ujao ni msimu wake wa pili sasa kucheza Ligi Kuu alianza na Majimaji ambayo imeshuka daraja na sasa anakipiga Kagera Sugar ambayo ipo nafasi ya 17 inapointi 43 ikiwa imecheza michezo 37.

Nafasi iliyopo Kagera ikiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Mbao endapo itakubali kichapo ugenini basi itakuwa imejiandikia tiketi ya kushuka daraja na mchezaji huyo kuingia katika rekodi nyingine ya kushusha datraja timu anazocheza.

Kapera mwenye mabao 9 katika ligi ya msimu huu anatarajia kuukosa mchezo wa mwisho wa ligi unaotarajiwa kuchezwa kesho dhidi ya Mbao jijini Mwanza kutokana na kukabiliwa na adhabu ya kadi tatu za njano.

Tetesi za usajili wake Simba zinaweza kumuengua kinda Adam Salamba ambaye atatakiwa kutolewa kwa mkopo katika timu zinazoshiriki ligi kuu ili aweze kwenda kukuza kiwango chake kutokana na kukosa namba ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kocha Patrick Ausems.


Share.

About Author

Leave A Reply