Sunday, August 18

Unaifahamu Pasaka?

0


By Kelvin Matandiko,Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Shamrashamra za maandalizi ya Wakristo kusherehekea kikukuu ya kufufuka kwa Mwana wa Mungu, Yesu Kristo zinaendelea. Lakini je unaifahamu maana ya Pasaka?

Mwananchi Digital kwa msaada wa mitandao inakufamisha kuwa, Pasaka ni sikukuu inayobadilika tarehe yake katika kalenda ya kawaida kila mwaka.

Pasaka ni sikukuu muhimu katika dini za Uyahudi na Ukristo. Jina la Pasaka limetokana na neno la Kiebrania “פסח” (tamka: pasakh).

Pasaka ya Kiyahudi ni ukumbusho wa ukombozi wa Wanaisraeli kutoka Misri wakati wa Musa mnamo miaka ya 1200 KK.

Pasaka ya Kikristo ambayo itasherekewa kesho duniani kote ni ukumbusho wa kufufuka kwake Yesu Kristo siku ya tatu baada ya kusulubiwa kwake. Inahesabiwa kuwa sikukuu muhimu kabisa katika ukristo.

Taarifa za Agano Jipya zinatoa habari ya kuwa kufa na kufufuka kwa Yesu kumetokea wakati wa sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi. Kwa hiyo jina la sikukuu hiyo limeendelea kutumika kwa ajili ya sherehe hiyo ya kikristo.

Share.

About Author

Leave A Reply