Thursday, August 22

UN itasimamia utokomezaji wa Ebola huko DRC

0Umoja wa Mataifa sasa ndio utasimamia harakati za kupambana na ugojwa wa Ebola huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC ili kuhakikisha unatokomeza kabisa ugonjwa huo ambao hadi sasa umeshawaua watu wengi na huku kukiwa na hatari ya kusambaa katika nchi jirani.

Hatua hiyo ya kuiomba Umoja wa Mataifa usimamie juhudi za kupambana na ugonjwa wa Ebola zimechukuliwa huko Geneva kufuatia ongezeko la vifo vya kila mara vya Ebola katika eneo la Kivu kaskazini pamoja na Ituri huko mashariki mwa DRC kwenye mji wa Butembo mahala ambako kumeshuhudiwa vifo na maambukizi mengi kwa wakazi wa huko.

Akizungumza na mwandishi wa VOA mbunge wa Beni, Kizerbo Kasereka alieleza kwamba alipokea kwa furaha taarifa za Umoja wa Mataifa kuingilia kati kusimamia utokomezaji wa ugonjwa wa Ebola katika eneo lao.

Share.

About Author

Leave A Reply