Monday, August 26

Uganda wapigwa jeki AFCON

0


By CHARLES ABEL

SERIKALI ya Uganda imetia chachu maandalizi ya timu ya Taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwezi ujao huko Misri, baada ya kuipatia Sh2.4 bilioni ili kugharImia maandalizi hayo.

The Cranes iliyopangwa kundi A la mashindano hayo sambamba na Misri, Zimbabwe na DR Congo, itaweka kambi huko Abu Dhabi kwa ajili ya maandalizi ya fainali hizo zitakazoanza Juni 19 hadi Julai 21.

Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa hundi ya fedha hizo za Uganda kiasi cha Sh4.7 bilioni sawa na Sh2.4 bilioni za Kitanzania, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda (FUFA), Injinia Moses Magogo, alisema fedha hizo zitasaidia kuiandaa vyema timu ya taifa.

“Namshukuru Mheshimiwa Rais, Yoweri Museveni, Waziri wa Elimu na Michezo, Mama Janet Museveni, Baraza la Taifa la Michezo na idara nyingine za serikali kwa juhudi kubwa waliyofanya na kutupa fedha hizi.

“Tunafurahi kupokea fedha hizi kwa wakati kutoka serikalini katika kipindi ambacho timu zetu za taifa tayari zipo kambini kujiandaa na mashindano ya kimataifa ambayo yako mbele yetu,” alisema Magogo.

Uganda imeita vikosi viwili vya timu ya taifa na kimoja ni kwa ajili ya maandalizi ya AFCON na kingine ni kile kitakachoshiriki mashindano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) ambayo yote yatafanyika mwezi ujao.Share.

About Author

Leave A Reply