Monday, August 26

Uchaguzi Malawi ushindani mkali

0


By Mwandishi Wetu na Mashirika

Lilongwe. Raia wa Malawi leo wamepiga kura kumchagua rais mpya katika uchaguzi ulikuwa na ushindani mkali kati ya wagombea watatu, miongoni mwa saba wanaowania nafasi hiyo ya juu.

Rais Peter Mtharika (78) ni miongoni mwa wanaowania nafasi hiyo ikiwa ni muhula wake wa pili, akiwa anapambana na makamu wake, Saulos Chilima na Lazarus Chakwera.

Mshindi anahitaji kuwa kura zaidi ya asilimia 50 ya kura zote. Mutharika alishinda muhula wa kwanza mwaka 2014 kwa kura asilimia 36.4.

Karibu wapigakura milioni saba waliojiandikisha walikuwa pia wanachagua wabunge na madiwani.

Kwa mujibu wa BBC miongoni mwa waliojiandikisha ni vijana chini ya miaka 34 na kura yao inaweza kuwa athari kubwa kwenye uamuzi.

Katika vituo vya kupigia kura kulikuwa na misururu mirefu karibu nchi nzima na wengi wa wapigakura walifika vituoni kabla hakujakucha ili waweze kutimiza jukumu hilo na kurejea majumbani. Siku ya uchaguzi nchini Malawi ni mapumziko.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa 12:00 asubuhi na vinatarajiwa kufungwa saa 12:00 jioni.

Mgombea mwenye ushindani wa karibu zaidi kwa Mutharika ni Chilima (46) anayewania kupitia chama cha Democratic Progressive (DPP), ametumia ushawishi kwa vijana akitumia karata ya kukosekana ajira. Hata hivyo, vyombo vya habari vimewanukuu wakosoaji wakisema haya yeye hataweza kuwapatia ajira zaidi ya milioni moja katika mwaka wake wa kwanza kama anavyodai.

Mapema alishindwa kupiga kura baada ya jina lake kutoonekana katika daftari katika kituo alichojiandikisha mjini Lilongwe. Hata hivyo baada ya kuwasiliana na maofisa wa Tume ya uchaguzi alipiga kura.

Share.

About Author

Leave A Reply