Saturday, August 24

Tuhuma 157 za rushwa zapokelewa Zanzibar

0


By Haji Mtumwa, Mwananchi [email protected]

Unguja. Kuanzia 2018 hadi Machi, 2019 Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar  (Zaeca) imepokea tuhuma 157 za makosa mbalimbali yakiwemo ya kuomba na kupokea  rushwa.

Makosa mengine ni matumizi mabaya ya ofisi na mali za umma, kukwepa kodi na rushwa katika zabuni.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Mei 20, 2019 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Issa Haji Ussi Gavu wakati akiwasilisha hotuba ya  makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya ofisi hiyo mwaka 2019/2020.

Gavu amesema kati ya tuhuma hizo,  majalada 31 yamefikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa hatua za kisheria na kupelekwa mahakamani.

Share.

About Author

Leave A Reply