Friday, July 19

Torres: Nimetwaa kila kitu maishani

0


Tokyo, Japan. Mshambuliaji nguli wa Hispania, Fernando Torres, ametamba kuwa hana alichokikosa katika maisha ya soka ndiyo maana amekubali kutua Sagan Tosu ya Japan.

Torres alitamba kuwa ametwaa kila kitu katika maisha ya soka barani Ulaya ndiyo maana akakubali kuondoka Atletico Madrid na kujiunga na timu hiyo ya Ligi Kuu Japan.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool, Chelsea, AC Milan na Atletico Madrid alisema anaamini katika mafanikio ya kisoka hana alichobakisha ndiyo maana amekuwa radhi kucheza katika ligi isiyo na umaarufu.

“Ligi Kuu ya Japan kama zilivyo nyongine za bara la Asia, ni tofauti sana na ile ya Ulaya haina ushindani nimekubali kuja huku kwa sababu naamini nimetwaa kila taji maishani,” alisema Torres.

Torres alitwa taji la Mataifa ya Ulaya 2008 na Kombe la Dunia mwaka 2010 akiwa na kikosi cha Hispania, pia alitwaa mataji yote makubwa ngazi ya klabu akiwa na Chelsea na Atletico Madrid.

Alisema mafanikio hayo ndiyo yaliyomfanya kukubalia ofa ya kukipiga nchini Japan ambako alitua katika usajili wa kiangazi mwaka huu akicheza soka la kujifurahisha na kujitengenezea maisha.

Share.

About Author

Leave A Reply